Siasa

MTALII KUTOKA BONGO

Hapa nilipo umeme na maji uwa hayakatiki, hamna vumbi wala harufu ya dampo. Wapi kwingine kwenye sifa kama izo kama sio Ulaya? Naona nazidi kukuchanganya acha nikulaisishie niko UBALOZI wa MAREKANI. Nikikuambia nina bahati huezi kunielewa mpaka uone umati wa watu nje. Wote wamekatwa bogi wameambiwa wajaribu siku nyingine. Niko kamili na mabegi yangu mgongoni. Yani wakinigongea viza tu nawahi uwanja wa ndege.

Wazo la kwenda kutalii nje limenijia jana tu na ghafla nikajiuliza ikiwa wazungu wanakuja afrika kutalii kwa nini na sisi hatuendi kwao kutalii? Unaambiwa swali lilinisumbua mpaka ninamua leo nidamkie hapa ubalozini. Unajua hakuna hata mswahili mmoja anayekwenda sijui Serengeti, sijui manyara au mikumi eti kwenda kuangalia wanyama tumekuwa tukilala na mbuzi na ng`ombe. Kila siku tunakoswakoswa na fisi tukienda kisimani. Ivi tofauti ya swala na mbuzi ninayemchunga kila siku ni ipi?

Ane wei tusipoteze muda kwa blah blah. Nipo chumba cha mahojiano ya VISA. Tupo watahiniwa kumi hivi wote ukituangalia ni mashujaa, makomandoo. Wakati nimekaa hapo kijana akitokea dirisha la mahojiano akilia machozi kama mtoto mdogo. Sikutaka kujua nini kinamsumbua maana bongo matatizo mengi labda kapata habari za msiba au katumiwa majibu ya ukimwi kwa njia ya meseji.ntajuaje!.

“Zumbukuku Saidi” mwanaume nikajizoa zoa mabegi yangu na kuelekea dirishani huku roho ikinidunda. Hofu kubwa ni kimombo. Sijui hata cha kuombea maji. Dirishani mzungu anyeidhinisha viza akawa ameshajua tatizo langu. “mambo vipi mshikaji” jamaa akanisalimia “poa” nikampa kumbe jamaa Kiswahili anakijua kuliko hata mimi. Kakaa miaka 10 halafu maneno ya mtaani kafundishwa na nyumba ndogo yake ya manzese.

“Marekani unaenda kufanya nini?” Mzungu akaniuliza “kutalii”nikajibu kwa kujiamini. “Marekani hakuna wanyama wala mbuga, unaenda kutalii nini”? sitaki kuona wanyama wala mbuga nataka kuona mahali yalipolipuliwa maghorofa kwa ndege. Nataka kwenda kumuona shwaziniga na Rambo wanapoishi na kutembelea kiwanda cha fubu.

Benk stement unayo? Mmarekani akaoji. Ni nini hiyo? Nikauliza… una shilingi ngapi” mzungu akaona anirahisishie. Kwa mazoea ya ya wabongo nikajua mzungu anataka kunitoa upepo! “Hatuwezi kukupa visa kabla hatujajua una uwezo wa kujigharamia huko uendako” nimejiandaa vya kutosha mbali na tiketi ya kwenda na kurudi nina dola mia mbili” Zumbukuku laki nne ni pesa ya kulala na kula hotelini siku moja tu hotelini. “mheshimiwa mimi ntakula kwa mamantilie na kulala kwa washikaji” hiyo ni mbaya kwa uchumi wan chi mtalii anapaswa kuinua uchumi wa taifa sio kubana matumizi kwa kula na kulala kwa washikaji. “ah mbona hapa kuna watalii wa kizungu wanashindia madafu na kulala vichochoroni” nikaona mzungu ameosa la kusema “ una ndugu marekani?” sina

Zumbukuku tutaakikishaje kama utaludi? “jamani tiketi ya kurudisi hii nnayo” TIKETI SIYO KITU WATANZANIA MMEZOEAKUZAMIA KUTAFUTA MAISHA BORA ULAYA. “wanaozamia ni wale ambao hawasomi magazeti na kusikiliza habari. Rahisi kikwete ameahidi maisha bora kwa kila mtanzania. Nikimbie maisha bora nimwachie nani?

Ghafla nikaona ananyanyua mhuri mkubwa na kuigonga passport yangu, roho ikatulia kwamba hatimaye pamoja na kuniweka kitimoto hatimaye ananipa VISA! Akaingiza pasi yangu kwenye shimo la dirisha nikaichukua huku nikitabasamu. “Tutaonana” akaniambia.
Kwani na wewe unakuja marekani? Nikamwuliza. “Hapana tutaonana manzese”

Kuangalia pass yangu vizuri nikagundua kuwa kanigongea mhuri wa kuninyima viza. “ Maombi yako yanatia mashaka sijapata kusikia mtalii anaenda kuona maghorofa. TEMBELEA MIKUMI UJIVUNIE UTAIFA KAKA.

KA IYO NDUGU YANGU NIMEBADILI KAMPENI, “TWENDENI TUKATALII BONGO”

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents