Promotion

MultiChoice Tanzania yaibuka kidedea Sabasaba (+picha)

Kampuni ya MultiChoice Tanzania imeipuka kidedea na ushindi wa cheti cha banda bora kwenye maonesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam.

1
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (Kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana cheti na kombe baada ya banda la DStv kuibuka kidedea katika kundi la waonyeshaji wa huduma na bidhaa za teknolojia ya Mawasiliano.

MultiChoice wameshinda cheti cha banda bora kwa upande wa mabanda ya bidhaa za Teknolojia ya Mawasiliano kupitia banda lao la DStv.

3
Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania akiwa na balozi maalum wa DStv, Nancy Sumari wakionyesha cheti na Kombe walivyokabidhiwa kampuni ya MultiChoice Tanzania baada ya kuibuka banda bora katika kundi la waonyeshaji wa huduma na bidhaa za teknolojia ya Mawasiliano katika maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
2
Wafanyakazi na mawakala wa MultiChoice Tanzania wakishangilia ushindi mara baada ya banda lao la DStv kuibuka banda bora katika kundi la waonyeshaji wa huduma na bidhaa za teknolojia ya Mawasiliano katika maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents