Michezo

Naomi Osaka atinga fainali za Indian Wells kibabe baada ya kumtoa mchezaji namba moja kwa ubora duniani

Mchezaji tennis raia wa Japani, Naomi Osaka amefanikiwa kuingia hatua ya fainali ya michuano ya BNP Paribas Indian Wells baada ya hapo jana siku ya Ijumaa kumtoa mwanadada Simona Halep  katika hatua ya nusu fainali.

Mchezaji tennis raia wa Japani, Naomi Osaka

Osaka anayeshika nafasi ya 40 katika viwango vya ubora wa mchezo huo duniani amemtoa, Simona Halep ambaye yupo nafasi ya kwanza katika viwango hivyo kwa ushindi wake wa seti 6-3 6-0.

Wachezaji tennis Naomi Osaka (kulia) na Simona Halep (kushoto) wakipeana mikono

Sasa mchezaji huyo anajipanga kukabiliana na Daria Kasatkina hatua ya fainali ambaye kwa upande wake naye alimfungashia virago Mmarekani Venus Williams hatua ya nusu fainali kwa jumla ya seti 4-6 6-4 7-5.

Baada ya kutolewa na Osaka katika hatua hiyo ya nusu fainali, mchezaji tennis anayeshika nafasi ya kwanza kwa ubora duniani kwa upande wa wanawake, Simona Halep amesema kuwa hakuwa mchezoni kabisa.

Sikujiskia kucheza, nilikuwa nje ya mchezo nilicheza vema hadi 4-3 lakini baada ya hapo nikatoka nje ya mchezo.

Mpinzani wangu alikuwa vizuri na mwenye kujiandaa kwa kiasi kikubwa na alikuwa na utayari wa kucheza na kushinda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents