Burudani

Nyoshi El Sadat asema vyombo vya habari vimeutupa muziki wa dansi nchini

Kiongozi wa bendi ya FM Academia, Nyoshi El Sadat amesema changamoto kubwa inayowakumba wasanii wa muziki wa dansi nchini ni kutengwa na vyombo vya habari.

Nyoshi_5

“Kuna matatizo kidogo yamejitokeza kutokana na media inafanya kama inatutupa sisi wanamuziki wa dansi,” Nyoshi aliiambia Bongo5.

Pamoja na hivyo muimbaji huyo amesema wanaendelea kujituma na kufanya kazi nzuri.

Alisema kama wasanii wengine na wao wanapenda kutafutwa na vyombo vya habari na kuhojiwa ili kusikika kwenye redio, kuonekana kwenye TV na kusomwa kwenye magazeti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents