Michezo

Pambano langu na Anthony Joshua litakuwa lakihistoria – Haye

Bondia raia wa Uingereza, David Haye anaamini pambano lake dhidi ya Anthony Joshua litakuwa kubwa na la kipekee ambalo halijawahi tokea katika ardhi ya nchi hiyo.

Bondia raia wa Uingereza, David Haye

Haye, anahitaji kucheza na Anthony Joshua hapo mwakani katika pambano ambalo anaamini litakuwa kubwa haijawahi tokea nchini Uingereza hii ni mara baada ya kurudi katika ulingo.

Bondia huyo wa uzito wa juu anatarajia kurea tena ulingoni mwaka huu baada ya kupona majeraha aliyo yapata wakati wapambano lake dhidi Tony Bellew mwezi Machi.

Bellew (kulia) akimpiga bondia Haye (kushoto) katika raundi ya 11 mwezi Machi 

Makubaliano yanaendelea kwaajili ya mchezo wa marudiano kati ya bondia huyo dhidi ya Bellew pambano linalotarajiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu ili kujiweka sawa kwaajili ya pambano lake na Joshua 2018.

“Lengo langu ni kurejea kabla ya mwisho wa mwaka huu na hilo ndilo ninalotarajia”,amesema Haye .

David Haye mwenye umri wa miaka 36, ameongeza kuwa ,”Nahitaji mapambano manne makubwa ndipo niamini kuwa naweza kupambana na mtu sahihi bondia namba moja kwangu, Anthony Joshua”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents