Michezo

Picha: Jezi mpya za Uingereza kuelekea kombe la dunia zavuja

Jezi mpya ya timu ya taifa ya Uingereza inayotarajiwa kuvaliwa wakati wa mashindano ya kombe la dunia nchini Urusi zimevuja kupitia mitandao ya kijamii.

Kampuni ya Nike ilitarajia kuzindua jezi hizo mpya kabla ya mchezo wao ujao wa kimataifa mwezi Machi, lakini kupitia mtandao wa FootHeadlines.com umeweza kuonyesha picha za uzi huo mpya wa Uingereza.

Jezi hiyo mpya inaonyesha wanyama aina ya Simba wa rangi ya blu, ufito mwekundu maeneo ya shingoni na nembo ya nike ya rangi ya bluu.

Timu ya taifa ya Uingereza inatarajia kucheza michezo ya kirafiki na Holland na Itali mwezi ujao ikiwa ni maandalizi kuelekea michuano ya kombe la dunia  inayofanyika nchini Urusi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents