Habari

Mhe Tundu Lissu atembelewa na ugeni mzito Ubelgiji

Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Mhe. Tundu Lissu ametembelewa na ugeni mzito leo Jumatatu Februari 5, 2018 huko nchini Ubelgiji akiwa katika matibabu.

Mhe Lissu akiwa na Maofisa kutoka Umoja wa Ulaya.

Mhe. Lissu ametembelewa na ugeni kutoka Makao Makuu ya Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa ajili ya kumjulia hali, amethibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

“Leo nimetembelewa na maofisa watatu kutoka Makao Makuu ya Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa ajili ya kunijulia hali na mazungumzo juu ya masuala mbali mbali yanayoihusu nchi yetu.

Ujumbe wa EU umeongozwa na Mkuu wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki katika Wizara ya Nje ya EU, Bw. Patrick Simonnet.

Pichani kutoka kushoto ni Bw. Patrick Simonnet; mke wangu Alicia; Mkuu wa Desk la Tanzania katika EU, Bi Marta Szilagyi; mimi mwenyewe; Bi. Hortensia May Lyatuu na Bi. Vania, ambaye ni afisa wa Ubalozi wa EU Tanzania anayeshughulikia masuala ya utawala bora na haki za binadamu.”

Mhe. Lissu aliondoka nchini Kenya mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu kuelekea nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi.
Soma zaidi – Mhe. Tundu Lissu awasili salama Ubelgiji, Ulinzi waimarishwa (+picha)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents