BurudaniUncategorized

Pre-Birthday Party ya Diamond ni full burudani (Full Video)

Msanii wa muziki kutoka WCB, Diamond Platnumz usiku wa kuamkia Jumamosi hii amefanya Pre-Birthday Party ndani ya ukumbi wa Element Club Masaki Jijini Dar es salaam.

Muimbaji huyo ambaye ni balozi wa kinywaji cha Belaire, aliambatana na team yake nzima ya WCB na wasanii wake, rapa Fid Q pamoja na County Boy na wote walipata fursa ya kuzungumza kidogo na kutoa burudani kwa mashabiki.

Akiongea na mashabiki waliojitokeza kwenye ukumbi huo, Meneja wa Diamond, Sallam amesema ndani ya wiki hii nzima Diamond atakuwa akifanya party za aina mbalimbali kuikarisisha 2/10/2017 ambayo ni siku ya birthday yake.

“Jamani leo tumeanza hapa, kesho tena kuna party, Jumapili napo tunaparty mpaka siku ya tukio Jumatatu,” alisema Sallam.

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Hallelujah akiwa amelishirikisha kundi la Morgan Heritage.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents