Bongo Movie

Ray vs Kanumba

 

Katika kile kinachoonekana ushindani wa hali ya juu wasanii wawili nguli wa filamu Vincent kigosi Ray na Steven Kanumba wameendelea na mashindano yao ambayo yanaonyesha yatachangia katika ukuzaji wa tasnia hiyo ya filamu.

Wasanii hao wa muvi bongo wanaonekana kwenda next level baada ya wote kuanzisha kampuni za kutengeneza filamu zao pamoja na kunua vifaa vya kisasa kabisa kuenda sambamba na shughuli hiyo.

Bongo5 ilipishana na Ray maeneo ya kinondoni vijana akiwa amekaa mbele ya gari yake ya production Toyota Town Hiace iliyorembwa na kupambwa kwa picha na jina la kampuni yake.

Aidha katika kufuatilia bongo5 imegundua pia Kanumba amejibua mashambulizi hayo siku chache tu  baadaye, ambapo na yeye alinunua na kulipamba gari lake aina ya town Hiace Toyota kwa ajili ya shughuli hizo hizo.

Wasanii hao pia wote wanamiliki mitandao yao ya habari yaani blogspot ambazo wanazitumia kama sehemu ya kujitangaza na kutoa habari

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents