Tragedy

Remmy Ongala Afariki Dunia

 

remmy
Habari za kusikitisha zilizofikia Bongo5 asubuhi hii ni kwamba msanii maarufu hapa Tanzania mwenye asili ya kiZaire, Dr. Remmy Ongala, amefariki dunia.

Inasadikika kwamba Ongala alipelekwa hospitali kuu ya Muhimbili jijini Dar es salaambaada ya kuzidiwa usiku wa Jumapili. Alitangazwa marehemu mapema Jumatatu baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya na madaktari kushindw kumsaidia.

Remmy Ongala atakumbukwa zaidi kwa ustadi wake kwa kupiga guitar na uimbaji wake ambao uliweza kuzivuta hisia za wengi kwa miaka 30 aliyokuwa akishughulika na muziki.

Tunaiombea familia ya Dr. Ongala faraja na Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents