Picha

Shambulio la bomu laua watu 30 harusini Uturuki

Shambulio la bomu lililoilenga sherehe ya harusi iliyokuwa ikifanyika nje, kusini mashariki mwa Uturuki, limesababisha vifo vya zaidi ya watu 30 na wengine 94 kujeruhiwa Jumamosi hii.

TURKEY1-master768

Naibu Waziri Mkuu, Mehmet Simsek, alisema kuwa shambulio hilo lililotokea kwenye mji wa Gaziantep, karibu na mpaka wa Syria, limeonekana kusababishwa na mtu aliyejitoa mhanga. Maafisa wengine wanadai kuwa shambulio hilo linaweza kuwa limefanywa na wanamgambo wa kikurdi au kundi la Islamic State, ISIS.

Picha zilizopigwa baada ya mlipuko huo, zimeonesha miili kadhaa ikiwa imefunikwa na mashuka maupe.

Hivi karibuni Uturuki imekuwa ikikumbwa na mashambulio ya kigaidi. June, watu waliokuwa na silaha na mabomu walishambulia uwanja wa ndege wa mji mkuu, Istanbul na kuua zaidi ya watu 40.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents