Michezo

Simba Sc yaifunga Stand United 2-1 na kurejea kileleni

Mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara baina ya klabu ya Simba Sc dhidi ya klabu ya Stand United umemalizik\a katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, kwa klabu ya Simba kuchomoza na ushindi wa magoli 2 kwa 1 dhidi ya Stand United.


Wachezaji wa Simba Sc dhidi ya Stand United matokeo 2-1.

Wanguja wa magoli hayo kwa upande wa klabu ya Simba ni mchezaji Juma Luizio anayecheza kwa mkopo kutoka Zesco United ya Zambia, aliyefunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya winga Shiza Kichuya.

Juma Luizio tena akawainua vitini mashabiki wa Simba kwa kufunga bao la pili na la ushindi dakika ya 35, kwa mara nyingine akimalizia kazi nzuri ya Kichuya.


Mchezaji wa Simba Mavugo akiwa na mcezaji wa Stand United, Simba 2 Stand United 1.

Kipindi cha pili milango ilikuwa migumu kwa pande zote mbili na Simba ikafanikiwa kuvuna pointi tatu kwa ushindi wa 2-1 na kurejea kileleni wakati kwa upande wa stand united mfungaji wa goli alikuwa Suleiman Kassim ‘Selembe’ aliyefunga sekunde ya 58 dakika ya kwanza.

Wekundu wa Msimbazi wanafikisha pointi 65 baada ya ushindi wa leo wakiwa wamecheza mechi 29, mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 62, ambao wanaweza kurudi kileleni kwa mabao zaidi, wakiifunga Mbeya City kesho Uwanja wa Taifa.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents