Uncategorized

Simba Yaifunga Azam Na Kutwaa Ngao Ya Hisani

Timu ya soka ya Simba Sports Club jana jioni iliweza kulitwaa kombe la Ngao ya Jamii baada ya kuichapa timu ya soka ya Azam FC magoli matatu kwa mawili katika pambano la kuashiria msimu mpya wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara kwa mwaka 2012/2013 wa kugombea ngao ya hisani.
Timu ya am ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake hatari John Bocco baada ya kufunga kwa kichwa baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Kipre Tcheche.
Azam ilicharuka tena katika dakika ya 36 ya mchezo mchezaji kipre Tcheche ambaye jana alikuwa katika kiwango kizuri alipiga bao la pili baada ya John Bocco kudhaniwa kuwa ameotea. Simba walicharuka na kupata bao la kusawazisha dakika chache kabla ya mapumziko baada ya beki wa Azam Said Morad kunawa mpira katika eneo la hatari na hivyo refa kuamua ipigwe penati ambayo ilifungwa kwa ustadi na mchezaji wa kimataifa wa samba kutoka Ghana Daniel Akkuffor.
Baada ya mapumziko Simba ilijikusanya na kurudi na nguvu upya ambapo mchezaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi ambaye alikuwa akishirikiana vema na Mrisho Ngasa vizuri na kufanikiwa kufunga goli la kusawazisha katika dakika ya 69 na kuamsha shangwe katika Jukwaa la mashabiki wa Simba ambao kabla ya goli hilo walikuwa kimya kwa muda mrefu.
Goli hilo liliamsha ari na morali ya wachezaji wa Simba kupambana kwa nguvu zote baada ya kuonekana kama walikuwa hawana lolote mbele ya Azam na kufanikiwa kupata goli la tatu na la ushindi katika dakika ya 78 ya mchezo ambapo kiungo mchezeshaji Mwinyi Kazi Moto aliipatia timu yake ya mtaa wa msimbazi Simba goli la tatu na la ushindi na kuamsha furaha iliyoje katika uwanja huo ambapo mashabiki wa Simba walijitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao.
Baada ya mchezo huo timu ya Simba walikabidhiwa kombe la Ngao ya hisani na Naibu waziri wa Kazi na Ajira Mh Mokongoro Mahanga.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents