Mitindo

Sio lazima High Heels, Flat Shoes pia ni bomba zaidi kwa wanawake wanene

Sio wanawake na warembo wote wanaweza kutembelea viatu virefu (High Heels). Karibu katika ulimwengu wa mitindo kutoka hapa Bongo5.

Mara nyingi wanawake hawapendi kupitwa na vitu hasa linapokuja suala la fasheni, leo tutatizamia viatu visivyo na kisigino kirefu hivi huitwa Flat shoes.


Flat shoes ni viatu ambavyo kila mwanamke analazimika kuwa navyo kwani humfanya awe mwepesi hata mwenye uharaka zaidi kwani visigino vyake huwa vyepesi na vya chini.

Kwa wanawake wa leo wapo watakao kuambia sina viatu flat ila huo ni uongo uliotukuka kwani kazima atakuwa navyo tu katika pair za viatu vyake.

Watu wenye miili mikubwa huwa na idadi kubwa ya viatu hivyo (Flat Shoes) kulinganisha na wale wenye miili midogo. Watu wenye miili mikubwa ni mara chache sana kuwa na viatu virefu kwani vinawafanya wawe huru(Balance) zaidi katika harakati zao kulinganisha na viatu virefu.


Vile vile viatu flat vipo ambavyo huvaliwa katika mitoko ya usiku na pia hata Wedges hutumika sana kwa mtu mwenye mwili mkubwa kwani huwa na kisigino kinene na kinachoweza kubalnce mwili wake.

MUHIMU:
Sio kila flat shoes ni ya kununua kisa tu uongeze idadi ya viatu nunua viatu vilivyo imara na vinavyoendana na hali ya hewa pamoja na fasheni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents