Bongo Movie

Stive apata baraka za Wazaanaki na Chif Azabi huko Butiama

 

Stive_Nyerere
Yule nguli wa kuiga sauti ya viongozi nchini, Stive Nyerere ambaye kwa sasa amejikita kwenye filamu za siasa na uchumi, ametoa taarifa kwa watanzania kwa kusema amefika salama Butiama na tayari ameshaanza michakato ya kurekodi filamu yake mpya ya Respect Nyerere.


Stive Nyerere amesema hakutarajia kama angepata ushiriano alioupata pande za huko Buatiama katika kuiandaa filamu hiyo, kwakuwa alihisi huenda watu wakawa hawajui chochote na ingekuwa tabu kwake katika kukamilisha filamu hiyo. Lakini amesema chaajabu wenyeji wamempokea kwa ukarimu sana na kushirikiana naye kwa hali na mali hasa baada ya kusikia amekuja kufanya filamu inayohusu maisha ya baba ya Taifa Mwalimu Julias Kambalage Nyerere. Kwanza wamempongeza kwa kusema ni jambo ambalo lilihitaji moyo wa kujitolea na uzalendo wa hali ya juu, kwani ni wasanii wachache sana wanaoweza kumwenzi baba wa Taifa kwa mtindo huu.

 

Pia wanakijiji kutokana na shangwe walimshauri na  kumuonyesha shughuli ambazo  mwalimu alipenda kufanya anapokuwa shambani au anapotoka shambani kwake.
Stive amesema ingawa mama Maria Nyerere hawakumkuta, lakini wanakijiji waliweza kumpa ushauri na kumuonyesha kile ambacho baba wataifa alichokuwa akikifanya muda wote katika mazingira yanayomzunguka. Stive na wenzake pia waliweza kwenda hadi kwa chifu wa Azabi wa Waazanaki.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents