Tupo Nawe

SUDAN: Kichwa cha mrembo aliyechochea maandamano yaliyomng’oa Rais Al-Bashir kinatafutwa

Mwanamke aliyekuwa mstari wa mbele katika maandamano ya kumpinga aliyekuwa rais wa taifa la Sudan, Omar al-Bashir, Alaa Salah anatafutwa kwa wudi na uvumba na baadhi ya wanajeshi ambao walikuwa wanamuunga mkono Rais huyo.

Alaa Salah

Alaa Salah (22) ambaye ni mwanafunzi wa uhandisi katika chuo kikuu cha kimataifa nchini humo (SIU) siku ya Jumanne kabla ya mapinduzi hayo, alionekana kwenye gari ndogo katikati ya Jiji la Khartoum akiandamana na waandamanaji wenzake na kupaza sauti za kudai demokrasia na utawala bora.

Imeelezwa kuwa picha yake baada ya maandamano hayo, ilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo limepelekea watu wengi wanaomuunga mkono Al-Bashir kumuwinda binti huyo.

Nilikaa juu ya gari ili kupasa sauti kwa wananchi wenzangu juu ya hali ya utawala mbovu. Ama hakika tulihitaji mapinduzi ya kidemokrasia na tumeweza sio kwa maufaa yetu tu bali kwa mustakabali mpana wa vizazi vijavyo,“ameandika Alaa kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Alaa amejivunia umaarufu nchini Sudan sio tu kwa wanawake wenzie bali hata kwa wanaume kwani ni mwanamke wa kwanza aliyejitolea kufa na kupona kuungamiza utawala wa Rais Omar al-Bashir.

Kufuatia maandamano hayo, Jana Alhamisi Rais Omar alijiuzulu nafasi yake ya urais baada ya kukaa kwenye madarakani kwa takribani miaka 30.

Alaa amesema kuwa “Hakuna maandamano yanayoweza kukamilika bila mwanamke, hauwezi ukawa na demokrasia bila mwanamke. Siwezi kuogop[a watu wanaonitishia kuniua hii ni nchi yangu nitaendelea kuishi hapa na ninachojaribu kuomba kwa sasa ni uangalizi kutoka umoja wa mataifa,“.

https://twitter.com/i/status/1116002453189795842

Rais Omar al-Bashir ni moja ya marais kutoka Afrika ambao walishawahi kuperwa waranti wa kukamatwa na Mahakama ya uhalifu ya kimataifa ya The Hague, kwa madai ya kuhusika na mashafuko ya Sudani Kusini.

Hata hivyo, Bashir alikana mashtaka hayo ambapo Mahakama hiyo ilieleza kuwa Rais jeshi lake liliua watu 300,000 mnamo mwaka 2003 .

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW