Soka saa 24!

Taff bado hapajatulia

taff_swebeface
Hali imeendelea kuwa ngumu katika shirikisho la wasanii wa filamu nchini, baada ya shirikisho hilo kutokea mpasuka mkubwa kati ya wasanii ambao tayari wameshakuwa na jina ‘U super star’ , kwa kuonyesha mvutano wa wazi huku  tatizo kubwa likilindima kwenye midomo yao na masikio yao ni kuibiwa kwa kazi zao, kuingia kwa watu wasio kuwa na vipaji kwa lengo la kutawala rushwa ya ngono

 

Katika mkutano wa juzi uliofanya Kinondoni  vijana  Wasanii wa Mkoa wa Kinondoni waliitishwa kikao kwa wasanii mbalimbali wakiwemo kutokana wilaya ya Kinondoni, wakiongozwa na mwenyekiti wa kikao hicho Swebe, walijajadili mambo machache ambayo yanaikumba tasnia kwa sasa.

Kwakuwa walimwarika mwenyekiti wa shirikisho taifa  TAFF, walieleza lile duku duku lao kwa lengo la kufika mbele kabisa kwenye mamlaka yanayohusiana na tasnia hiyo.

taff_wasanii

Miongoni mwa mambo waliyoyatilia mkazo ni kudharauliwa kwa wasanii ambao wanaoonekana kama wachanga, wakati wapo kwenye sanaa kwa muda mrefu, kusambazwa kwa wasnii wenye majina peke yao, kukumbatiwa kwa wasanii wachache na kufanyiwa promo kwa video zao, mtandao wa magazeti ambao unaharibu tasnia.

Wasanii walichangia mada kwa kusema, watu ambao walianzisha Taff , na ndiyo hao hao waliokuja kuivunja na kuanzisha Bongo Moviel Club ambao wanasadikiwa hawalitambui shirikisho wala raisi wa shirikisho hilo. wasanii wengine walitoa kero zao za moja kwa moja kwa kampuni ya usambazaji wa filamu Tanzania ya Step.

wengine hawakuacha kutua shutuma zao kwa wasanii ambao walimeshajijengea jina kwamba wanatumia fedha ili kuuza sura kwenye magazeti.

taff_raisi

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW