FahamuHabari

Tanzania yakimbiza kwa wingi wa Tembo Afrika

Tanzania imetajwa kuwa inaongoza kwa idadi kubwa ya Simba, Nyati, na Chui ambapo inashika namba moja kwa Wanyama hao Afrika huku ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na Tembo wengi Barani Afrika hivyo kuchochea ongezeko la Watalii na kufikia malengo ya Seriiali ya kufikisha idadi ya Watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania TAWIRI Dkt. Eblate Mjingo wakati wa hafla ya kutangaza matokeo ya Sensa ya Wanyamapori na Uzinruzi wa Ripoti na Taarifa ya Watalii waliotembelea Nchini Tanzania mwaka 2023.

Akiwasilisha taarifa ya Watalii waliotembelea Tanzania mwaka jana, Mkurugenenzi wa Utafiti na Mafunzi Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Edward Kohi amesema kuna ongezeko la asilimia 118 ukilinganisha na ukuaji wa asilimia 96.2 Barani Afrika.

Akitoa maelekezo ya Serikali mara baada ya kuzindua ripoti hiyo na kupokea matokeo ya Sensa, Waziri wa Maliasili na Utalii Anjelah Kairuki ameelekeza Taasisi za Uhifadhi kuweka jitihada kuongeza Wanyama ambao wanapungua na kuhakikisha Tembo wanaoongezeka hawaleti madhara kwa Binafamu.

Sensa ya Wanyamapori Nchini Tanzania imefanyika katika mifumo mitatu ya ikolojia kati ya 11 iliyopo Nchini na inalengo la kukuza, kuendeleza utalii, Kupunguza migogoro kati ya Binadamu na Wanyamapori, sanjari na kusaidia utekelezaji wa mikataba ya uhifadhi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents