Habari

Toni Braxton na Babyface waungana kufanya album ya pamoja

Mwanzoni mwa mwaka huu (February) mwanamuziki mshindi wa tuzo 22 za Grammy, American Music, Billbord Music nk. Toni Braxton, alitangaza kustaafu kufanya muziki na kuhamishia nguvu yake katika uigizaji. Lakini inaonekana kuna kitu kimemshawishi kwenda tofauti na uamuzi huo sababu ametangaza kurudi studio kwaajili ya kurekodi album ya collabo.

tonibabyface

Toni Michelle Braxton (45) ametangaza kuungana na mwanamuziki mkongwe Kenneth Brian “Babyface” Edmonds (54) kwaajili ya kutengeneza album ya pamoja, kwa mujibu wa Billboard.

Hii itakuwa si mara ya kwanza kwa wanamuziki hawa kufanya collabo, Babyface aliwahi kushirikishwa katika album ya Braxton “Secrets,” iliyokuwa na hits kama “Un-Break My Heart.”

Wakati wawili hawa wako katika maandalizi ya kutoa album hiyo, kwa sasa Babyface yuko katika tour yake binafsi ya muziki, wakati Toni Braxton anategemewa kuanza tour yake ya North America (August) mwaka huu kwa mujibu wa Rollingstone.

Album hiyo inayotayarishwa na Motown Records inategemewa kutoka mwezi September mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents