Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Michezo

‘Tulichowafanya Simba tutawafanyia Azam FC’ – Kagera Sugar

By  | 

Kocha msaidizi wa Kagera Sugar Ally Jangalu amejitapa kuwa kikosi chake kipo imara kupambana na Azam FC mwishoni mwa juma hili huku akidai watapambana kuhakikisha wanabakia katika nafasi ya tatu ndani ya msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

 

Kocha huyo amesema japokuwa ligi imekuwa ngumu lakini wana matumaini makubwa ya kuwafunga wapinzani wao Azam FC waliowatangulia nafasi moja mbele katika msimamo wa ligi.

“Wachezaji wangu wote kiafya wapo vizuri,┬átangu tumeanza Ligi tumekuwa washindani mpaka hii leo tupo nafasi ya nne tukiwa tumepishana pointi mbili na wapinzani wetu Azam FC ambao wapo nafasi ya tatu na tunataka tushindane ili tuipate nafasi ya tatu. Kwahiyo tutafanya kile kile tulichokifanya kwa Simba“. Alisema Jangalu kwenye mahojiano yake na Bongo Five.

Mchezo huo wa kukata na Shoka utachezwa Jumamosi kunako dimba la Azam Complex.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW