Uchambuzi: Premier League kutimua vumbi wikiend hii (+Audio)

Ligi pendwa zaidi duniani, Premier League inatarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi wikiendi hii kwa msimu wa mwaka 2020/21 huku siku ya Jumamosi macho na masikio ya wapenda soka watayaelekeza pale Uingereza.

Jumla ya michezo minne itapigwa siku ya Jumamosi ya Septemba 12, lakini mashabiki waliyowengi watauangazia zaidi mchezo wa Washika bunduki Arsenal wakiwa ugenini dhidi ya Fulham na ule wa Mabingwa watetezi Liverpool watakapo wakabili Leeds United.

Mchambuzi wetu @abbas__pira amekiangazia kikosi cha Arsenal msimu huu baada ya usajili wao lakini pia Mabingwa watetezi wa Premier League, Liverpool.

Mechi nyingine zitakazopigwa siku hiyo ya Jumamosi kuachia hizo ni pamoja na Crystal Palace Vs Southampton na West Ham dhidi ya Newcastle.

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW