Burudani ya Michezo Live

United Airlines matatani kwa video ya abiria aliyeondolewa kwenye ndege kimabavu

Video mpya ya abiria aliyekuwa akiondolewa kimabavu toka kwenye kiti chake na kubuluzwa katika njia ya kupitia kwenye ndege ya shirika la United Airlines iliyokuwa imepandwa na abiria zaidi ya kiwango, imemuonesha mtu huyo akipiga kelele ‘niueni tu’ huku damu nyingi zikimtoka puani.

Tukio hilo lilitokea Jumapili jioni na limesababisha hasira kubwa mtandaoni. Maelezo ya polisi yanasema kuwa mtu huyo aliumia kutokana na kupigwa na polisi wa uwanja wa ndege kuvutwa kwa nguvu.

Abiria huyo mwenye umri wa miaka 69 alidai kuwa ni daktari. Hatua ya kuwashusha baadhi ya abiria ilitokana na ndege hiyo kuwa na abiria wengi kuzidi idadi inayotakiwa hivyo ililazimika baadhi yao kushushwa.

CEO wa kampuni hiyo ameomba radhi kufuatia tukio hilo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW