Video: Baada ya ‘Kisogo’ Gabo kaja na hii

Muigizaji wa filamu nchini Gabo Zigamba, aliyetoa filamu fupi ya ‘Kisogo’ akiwa na muigizaji Wema Sepetu, ameamua kukazia katika kuhakikisha soko la filamu linazidi kukua na kuwa na filamu bora na zenye uhalisia.

Muigizaji huyo kwa sasa yupo mbioni kuachia kazi yake mpya ya ‘Siyabonga’ huwenda ikaanza kuachiwa kwa njia ya mtandao kama alivyo fanya hapo awali.

Gabo kwa sasa ndiye msanii wa kiume anaeangaliwa zaidi na ameshatajwa na baadhi ya mashiki kuwa ndiye mrithi wa mikoba ya marehemu Steven Kanumba.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW