Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Video: kijana wa miaka 21 auawa na mama akijaribu kuiba watoto akiwa na bastola

Mama mmoja ambaye ni afisa wa jeshi la polisi nchini Brazil, Katia da Silva Sastre, 42, ameonyesha ushujaa wake katika siku ya Mama Duniani Jumamosi iliyopita ya April 12.

Katia alifanikiwa kumdhibiti kijana ambaye alikuwa akijaribu kuwachukua kinguvu watoto wadogo huku akiwa na bastola katika eneo ambalo walikuwepo kina mama wengi karibu na shule huko mjini Sao Paulo.

Katika tukio hilo kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Elivelton Neves Moreira, 21, alitoa bastola yake huku akimtishia mtu ambaye alitaka kumpora kwenye eneo hilo ndipo Katia ambaye alivaa nguo za kiraia alitoa bastola yake kwenye mkoba wake na kumfyatulia kijana huyo ambaye baadae alifariki dunia.

Kutokaa na tukio hilo la kishujaa alilolifanya Katia da Silva limemfanya kupata pongezi kubwa na zawadi kutoka kwa Gavana wa Sao Paulo, Márcio França.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW