Mitindo

Visura waingia kambini

FOTHatua ya pili ya mashindano ya Face of Tanzania yameanza jana baada ya kuchaguliwa kwa washiriki 18 kutoka mikoa mbali mbali hapa nchini, kwa kweli kuna visura tofauti tofauti. Washiriki wataingia kwenye kambi maalum na kuishi humo kwa muda wa mwezi mmoja na shughuli hizi zitakuwa zitarushwa hewani kupitia kituo cha luninga cha TVT.

Hatua ya pili ya mashindano ya Face of Tanzania yameanza jana baada ya kuchaguliwa kwa washiriki 18 kutoka mikoa mbali mbali hapa nchini, kwa kweli kuna visura tofauti tofauti.

 

 

 

Washiriki wataingia kwenye kambi maalum na kuishi humo kwa muda wa mwezi mmoja na shughuli hizi zitakuwa zitarushwa hewani kupitia kituo cha luninga cha TVT.

 

 

 

Kambi hiyo ambayo iko maeneo ya Bahari Beach itawakusanya washiriki wateule katika fainali hizo, watakuwa wakijifunza mambo mbali mbali kama vile tabia, majukumu na mambo mengi yanayohusiana na uanamitindo ikiwa ni pamoja na kujiamini, kuzijua sheria za mitindo n.k.

 

 

 

Katika kila hatua watakuwa wakitoka washiriki wawili kwa kupigiwa kura na watazamaji kwa njia ya kutuma SMS (ujumbe mfupi wa simu), mpaka watakapobakia washiriki kumi watakaoingia katika fainali ya mwisho kwa ajili ya kumsaka mshindi atakayejipatia bahati ya kusaini mkataba mkubwa na kampuni ya O Model Africa Modeling Agency iliyopo Johannesburg nchini Afrika Kusini inayomilikiwa na mwanamitindo maarufu Oluchi.

 

 

 

Itakapofika Jumapili ya tarehe 9 mwezi huu, onesho la washiriki hawa wakiwa huko kambini linatarajiwa kuoneshwa kupitia kituo cha luninga cha TVT kuanzia saa moja usiku, ambapo kitakuwa kikirushwa kila siku ya Jumapili na Jumatano saa moja usiku, na kurudiwa Jumatatu saa kumi jioni na Jumamosi saa nane mchana.

 

 

 

Unaweza kuona jinsi mashindano haya yasivyo na upendeleo kwani waandaaji wamewachukua wasichana kutoka katika mikoa tofauti ya hapa nchini akiwamo mmasai wa ukweli kabisa kutoka Arusha wilaya ya Monduli na wengine kibao kutoka mikoa tofauti.

 

 

 

FOT

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents