Siasa

Waliokufa Mgodini watazikwa kwa Heshima

RAIS Jakaya Kikwete amewahakikishia ndugu wa marehemu waliokufa katika mgodi wa tanzanite, Mererani, kuwa marehemu hao watazikwa kwa heshima

RAIS Jakaya Kikwete amewahakikishia ndugu wa marehemu waliokufa katika mgodi wa tanzanite, Mererani, kuwa marehemu hao watazikwa kwa heshima kama binadamu wengine.


 


Akizungumza na umati wa wachimbaji waliofurika katika uwanja wa kitalu B kwenye migodi hiyo jana, wakiwa na nyuso za simanzi, Rais alisema vikwazo vinavyozuia uopoaji kama ukosefu wa pampu vitashughulikiwa mara moja.


 


“Mwanadamu hupanga yake na Mungu akapanga yake … tutahakikisha vikwazo vinavyozuia kazi hii vinaondoka na wanazikwa kwa heshima zote,” alisema Rais.


 


Pamoja na kutoa pole kwa wafiwa, alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bw. Henry Shekifu na wataalamu kuangalia kiwango cha maji ndani ya migodi kwa siku mbili ili ifunguliwe na shughuli za wachimbaji zilizosimama tangu juzi zianze tena.


 


Kauli hiyo ilisababisha wachimbaji hao kushangilia kwani kilichokuwa kimejitokeza, ni kukosa matumaini ya maisha baada ya uchimbaji kusimamishwa.


 


Migodi hiyo hadi jana ilikuwa ikilindwa na skari wa kikosi cha kutuliza ghasia, huku ndugu wa marehemu wakijazana katika kila mgodi iliko miili ya ndugu zao wakitamani kuingia mashimoni bila kujali harufu kali.


 


Hadi juzi Rais anawasili eneo la tukio hakukuwa na mwili zaidi ya ile kumi iliyoopolewa, ingawa miili 13 ilishagundulika katika mashimo mbalimbali.


 


Hata hivyo hali katika eneo hilo, licha ya mashine kusukuma upepo migodini, ilikuwa bado ni mbaya huku harufu ya miili iliyoanza kuharibika ikiendelea kusambaa.


 


Wakati huo huo, Chama cha Wananchi (CUF) kimeeleza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa za maafa ya Marerani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents