Bongo Movie

Wastara unamulikia wenzio wakati unateketea – Florah Mvungi

Muigizaji wa filamu za Bongo, Florah Mvungi amemfananisha Wastara sawa na mshumaa unaoteketea ukiwaangazia watu kutokana na yale anayopitia katika maisha yake.

Hivi karibuni Wastara alielekea nchini India kwa ajili ya kupata matibabu ya mguu uliokuwa ukimsumbua kwa kipindi kirefu, hivyo Florah ni kama ameamua kumitia moyo..

“Kitu kizuri ni kwamba wewe ni wa furaha siku zote, umekuwa msaada kwa wengi tuu huku ukionyesha furaha yako kwa yote uliyowafanyia pasipo kujua kumbe nawe ulikuwa na maumivu makali, umekuwa mshumaaa unamulikia wenzio wakati nawe unateketea,” ameandika Flora Instagram na kuendelea.

“Mungu akutie nguvu na akupe uponyaji wa milele ili uishi ukiyafurahia maisha Dada yangu, msaada wako naujua mimi na siwezi kusahau, nakupenda, upone inshaallah urudi salama,” amesisitiza.

January 26 mwaka huu Rais Dkt. John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli walimchangia Wastara Tsh. Milioni 15 kwa ajili ya matibabu na February 4 ndipo aliondoka nchini kuelekea India.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents