Yohan Cabaye asaini klabu ya Al Nasr kutoka falme za kiarabu

Mchezaji wa klabu ya Crystal Palace ya Uingereza, Yohan Cabaye amesaini kandarasi ya miaka miwili na timu ya Al Nasr kutoka falme za kiarabu.

Cabaye amethibitisha hilo hapo jana siku ya Jumanne kupitia tovuti yake na mitandao ya kijamii huku usajili huo ukitoa alama kuwa ndiyo mwisho wa soka lake ndani ya klabu ya Crystal Palace baada ya kuitumikia kwa muda wa miaka mitatu.

Cabaye mwenye umri wa miaka 32, amesaini kandarasi hiyo ya miaka miwili yenye maskani yake nchini Dubai na kutarajia kuanza kuitumikia msimu huu unao kuja huku akipewa jezi namba 7.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW