Burudani

2 Face Awatembelea Washiriki Big Brother Africa Star Game

Msanii nguli wa muziki kutoka Nigeria 2 Face Idibia jana aliwashtua washiriki walio katika jumba la Big Brother wanaoendelea katika shindano la Big Brother Stargame 2012 baada ya kutokelezea katika mjumba huo na kuwa surprise ambayo hawakuitegemea.

2 Face aliingia katika mjumba huo majira ya mchana na kuamsha taharuki kwa washiriki waliomo ndani ya mjumba kwani hawakuamini walichokuwa wanakiona. Karibu washiriki wote walionyesha mshangao wa wazi kwa kutoamini wanachokiona baada ya kuambiwa hapo awali na Biggie kwamba wakusanyike nje kwenye bustani na kisha baada ya dakika kama tano wakashangaa mtu anatokea akiwa amepiga suti ya kijivu na miwani.

Baada ya kufika karibu yao washiriki hao walimtambua na kupiga yowe za furaha kwa kumuona amewatembelea ambapo walifikiri naye ni mmoja wa washiriki walianza kupiga nae stori kwa kumuuliza kama amekuja kujiunga nao kwenye shindano kwani walifikiri ni mmoja wa All Star. Kwa ucheshi 2 Face alisalimiana nao kwa kuwapiga hug na kisha kuongea nao.

Angalia Picha za ujio wake ndani ya Jumba

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents