BOB na Micharazo waanza ziara ya nchi nzima, inaitwa ‘Biz kwenye Game’
BOB na Micharazo wameanza ziara ya nchi nzima waliyoipa jina ‘Biz Kwenye Game.’ Ziara hiyo inaanza Ijumaa hii mjini Mtwara.
Akiongea na Bongo5, Nyandu Toz amedai kuwa tangu BOB na Micharazo waungane pamoja hawajahi kufanya ziara ya pamoja na hivyo mwaka huu wameamua kuwapa mashabiki kile walichokisubiri kwa muda mrefu.
“Mwaka huu 2016 tumeamua kuacha shughuli zote, Kabayser aache mambo yake, Becka aache shughuli zake, mimi niache shughuli zangu tuwe busy kwenye game. So ndio maana hii tour imeitwa Bob & Micharazo: Busy kwenye Game,” amesema Nyandu.
Amesema wameamua kuanza mikoa ya Kaskazini ambapo Ijumaa hii watakuwa Mtwara, Jumamosi Masasi na Jumapili Lindi.
Kwa upande mwingine Nyandu amesema BOB na Micharazo ni kundi ambalo limedumu kwa muda mrefu bila migogoro na kwamba mwaka huu wameamua kuwapa vitu vingi zaidi mashabiki wao.