Habari

Jamaa huyu wa Malawi analipwa kubikiri watoto ili kuondoa mikosi

Katika tamaduni nyingi kote duniani mwanamke anapoolewa huwa ni fahari kubwa sana akiwa ni bikira.
Mathalan ni dhihirisho la mwanamke kuwa amelelewa na kutunzwa vyema.

Ni dhihirisho la usafi.

Hata hivyo jamii moja nchini Malawi haithamini ubikira wa watoto wao wa kike.
Amini usiamini wazazi huwa wanamlipa ”Fisi” kumbikiri binti yao punde tu anapopata hedhi yake ya kwanza.

160721100547_aniva_the_hyena_624x351_bbc_nocredit
Aniva huchemsha mizizi hiyo kabla ya kuanza kubikiri watoto kwa takriban siku 3 hivi

Wanaamini kuwa binti ambaye ni bikira ni mkosi kwa jamii!
Malimwengu haya.

Wazazi na jamii kwa jumla katika maeneo mengi ya kusini mwa Malawi wamekuwa wakishikilia tamaduni hii kwa miaka na mikaka.
”Fisi” ama wanaume wanaowabikiri watoto wa kike huchaguliwa na wazazi kuwaondolea mikosi.

160721115506_malawi_districts_624.swahili

Na huwa ni sherehe kubwa inayomtangulia binti kupelekwa unyagoni kisha kuwatembelea shangazi wake kabla ya kujulishwa kwa fisi.
Amini usiamini hao mafisi hulipwa takriban dola $7 kwa kila kitendo cha ngono na hao mabinti ambao wengi huwa na kati ya umri wa miaka 11-14.

Fisi mmoja katika kijiji cha Nsanje, Eric Aniva ameiambia BBC kuwa hajui kwa kweli amewabikiri wasichana wangapi, kwa sababu ni wengi.

”Kwa kweli mimi nimewabikiri zaidi ya wasichana 104,” amesema. ”Hii ndiyo tamaduni yetu”.

160721100955_aniva_624x351_bbc_nocredit
Aniva na familia yake

Na huwa ni sherehe kubwa inayomtangulia binti kupelekwa unyagoni kisha kuwatembelea shangazi wake kabla ya kujulishwa kwa fisi.
Amini usiamini hao mafisi hulipwa takriban dola $7 kwa kila kitendo cha ngono na hao mabinti ambao wengi huwa na kati ya umri wa miaka 11-14.
Fisi mmoja katika kijiji cha Nsanje, Eric Aniva ameiambia BBC kuwa hajui kwa kweli amewabikiri wasichana wangapi, kwa sababu ni wengi.
”Kwa kweli mimi nimewabikiri zaidi ya wasichana 104,” amesema. ”Hii ndiyo tamaduni yetu”.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents