Habari

Rais Magufuli akabidhi uenyekiti EAC kwa Rais Museveni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemkabidhi rasmi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Rais Magufuli ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, ameishukuru Jumuiya ya EAC kwa kumwamini yeye na nchi ya Tanzania kwa kuwaongoza miaka miwili.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru kwa ushirikiano wenu na mkubwa kwa kuniamini mimi na nchi yangu kwa kipindi chote nilichokuwa kiongozi wa Jumuiya hii, Na mimi naomba nikabidhi kwa kaka yangu, Mzee wetu, Yoweri Kaguta Museveni, Mliniamini mkanichagua licha ya kuwa madarakani kwa muda mfupi,”amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Rais Museveni baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo, amesema ameishukuru Jumuiya hiyo kwa kumchagua na pia amemshukuru Rais Magufuli kwa kwa kuongoza Jumuhiya hiyo kwa miaka miwili.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents