Burudani

Nape, Afande wamlilia Tongolanga wa ‘Kila Munu Ave na Kwao’

Aliyekuwa Waziri Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye pamoja rapa Afande Selle wameonyesha kuguswa na kifo cha mwanamuziki wa zamani, Halila Tongolanga aliyefariki Jumatatu hii akiwa hospitali ya Muhimbili alipokuwa akifanyiwa matibabu.

Halila alikuwa amesafirishwa kutokea Ndanda kuja Muhimbili akihisiwa kuwa na matatizo ya figo. Licha ya kuwa alifika Muhimbili Ijumaa iliyopita usiku, lakini alikuwa hakufanyiwa vipimo vyovyote vikubwa mpaka umauti unamkuta.

Jumanne hii Nape ambaye pia ni mbunge wa Mtama, alitweet “Pumzika kwa amani kaka Tongolanga, umeutendea haki Utamaduni wetu, umekuwa mzalendo wa kweli! Nenda Pumzika kwa amani!,”

Naye rapa Afande Selle aliandika “Harilla Tongolanga….Chilambo Chabhene….Kila Munu Avena Kwao….Nilikua Na Marafiki Sikatai….Lkn Rafiki Wa Kweli BaiBai….RiP Mwlm Wa Muziki Wa Kwetu….Poleni WakuNtwara…Kumasasi Na Kunewala,”

https://youtu.be/Un53XqsIGrM

Mungu amlaze mahali pema peponi Halila Tongolanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents