Burudani

Kifafa cha katisha show ya Lil Wayne

Rapper kutoka Marekani, Lil Wayne amelazwa upya hospitalini baada ya kuanguka kutokana na ugonjwa wa kifafa aliyonao.

Wayne ambaye siku ya jana alikuwa na tamasha lake katika ukumbi wa Drais Beachclub mjini Vegas, alijikuta akiwa kitandani na kupelekea show yake kukatishwa baada ya kukutwa akiwa hana fahamu katika chumba cha Hoteli baada ya kuanguka kutokana na ugonjwa wa kifafa.

Kwa mujibu wa vyanzo viwili vya karibu zimeeleza kuwa rapper huyo amelaza katika hospitali ya Northwestern Memorial iliyopo mjini Chicago, baada ya kukutwa amepoteza fahamu katika chumba cha hotel ya Westin- Michigan Avenue.

Naye Daktari aliyekuwa akimtibua msanii huyo amemtaka apumzike kwa siku kadhaa ili afya yake iweze kurudi katika hali ya kawaida licha ya kuwa aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo siku ya jana(Jumapili).

Hii sio mara ya kwanza kwa msanii huyo kuugua na kuanguka kutokana na ugonjwa wa kifafa, pia msanii huyo aliwahi kukiri kuwa anatumia dawa za kuzuia hali hiyo isitoke mara kwa mara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents