Habari

Serikali yatoa onyo kali kwa watu wanaoendelea kusambaza picha za miili ya waliopata ajali ya moto mkoani Morogoro

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali,   Dkt. Hassan Abbasi, ametoa onyo kwa wananchi kuacha kusambaza picha za miili ya wananchi walioathirika na moto uliotokana na mlipuko wa mafuta yaliyokuwa kwenye lori lililopinduka asubuhi ya jana mkoani Morogoro.

Image result for msemaji wa serikali
Dkt. Hassan Abbasi

Dkt. Abbasi amesema: “Ni kinyume cha sheria na utamaduni wa Mtanzania kusambaza picha za watu wakiwa kwenye hali ya fadhaha”.

Dkt. Abbasi ametoa kauli hiyo jana Agosti 10, 2019 katika mahojiano maalum kupitia  Televisheni ya Taifa (TBC) kuhusiana na ajali hiyo.

Katika mahojiano hayo, Msemaji Mkuu wa Serikali amewaasa wananchi kuacha kusambaza habari zisizokuwa na uhakika ili kuepusha upotoshaji wa taarifa.

 

Niwaombe wananchi kuacha kusambaza habari za uongo kuhusu idadi ya vifo na majeruhi wa ajali.  Ni muhimu sana watumie vyanzo rasmi vya Serikali kupata taarifa hizo ambavyo kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro (RPC) Wibrod Mtafungwa” ameeleza Dkt. Abbasi.

 

Aidha Dkt. Abbasi ameviasa vyombo vya habari kufuata maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari sahihi na kupiga na kutumia picha zilizo na staha ili kuepusha taharuki katika jamii.

Ajali hiyo imetokea jana tarehe 10 Agosti, eneo la Msamvu mkoani Morogoro ambapo Lori lililokuwa limebeba shehena ya mafuta lilipinduka na baade kulipuka moto.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents