Habari

Dodoma: OSHA imewataka mafundi kuzingatia Usalama na Afya Mahalipa Kazi ili kujiletea maendeleo na kuongeza kipato chao(+Video)

Mafundi katika nyanja tofauti wametakiwa kuhakikisha wanazingatia usalama na afya wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao, kwani mtaji namba moja katika majukumu yao ni mfanyakazi.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahalipa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la mafundijijini Dodoma.

Bi Mwenda amesema katika jitahadi hizo za kujiletea maendeleo kwa mafundi hao wataweza kuboresha mazingira yao na hivyo kuongeza kipato kutokana na kuwa salama na kulinda afya zao

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Fundismart’ iliyoandaa kongamano hilo, Bwana Wiseman Luvanda, amesema lengo la programu ya ‘FundiSmart’ inalengo la kuwawezesha mafundi kutumia ujuzi na vipaji vyao ipasavyo iliwaweze kupata mafanikio na kuboresha maisha yao.

Naye kwa upande wake Mkaguzi toka OSHA Ndugu Venance Buliga amesema kuna matatizo mengi wanayoweza kuyapata, hivyo kuzingatia usalama kwa mafundi kutasaidia kuwawezesha kuwa salama wakati wote.

Nao kwa upande wao washiriki wa kongamano hilo hayo wamesema kongamano hili limewasaidia kupata elimu ambayo walikuwa wakiikosa, kwa kutoakujua namna ya bora ya kuweza kujikinga na madhara ya kufanya kazi kwenye mazingira ambayo sio salama

Programu ya Fundismart imebuniwa kwa lengo lakuwasaidia mafundi kuboresha kazi zao kupitia mafunzo mbalimbali ikiwemo elimu ya fedha na ujasiriamali, kuwapa msaada wakisheria pamoja na kuwawezesha kupata wateja kupitia App ya Fundsmart ambayo itakuwa na orodha yamafundi hao na hivyo kuweza kufikiwa kirahisi na wateja mbalimbali wanaohitaji huduma za kifundi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents