Habari

NMB sasa yawafikia wakazi wa Sinza – Dar es Salaam

NMB ikiwa ni benki ya chaguo la watanzania wengi, jana Machi 19, 2014 ilifungua rasmi tawi lake jipya maeneo ya Sinza Mori mkabala na kituo cha kuwekea mafuta cha ‘Big Born’ikiwa na lengo la kuwafikia wateja wake, ambapo takribani zaidi ya wateja 300 wamekuwa wakihudumiwa kila siku katika tawi hilo.

_DSC4688
Afisa Utumishi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Mugomi akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Sinza. Kwanza kulia ni ni Meneja wa Tawi la NMB Sinza Bi.Kidawa Masood na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam Bw. Salie Mlay wakishuhudia ufunguzi huu uliofanyika jana jijini Dar es Salaam

Tawi hili limeanza kufanya kazi hivi karibuni, ambapo limeonekana kuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi Sinza ikiwa ni moja kati ya maeneo yenye wakazi wengi jijini Dar es salaam.Hii itakua pamoja na mitaa jirani kama, Kijitonyama, Mabatini, Afrikasana,Tandale, Sayansi na maeneo mengine kwa kupata huduma za kibeki kwa uharaka zaidi.

Akizungumza katika ufunguzi huo, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Salie Mlay alisema lengo kubwa la kupeleka tawi hilo ni kuwapa huduma kwa ukaribu wateja wao waliopo katika eneo hilo. Alifafanua kwamba, tangu kuanzishwa kwake tawi hilo limekuwa ni mkombozi kwa wateja wengiwakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na watu mbalimbali. “Tawi letu linatoa huduma zote za kibenki, na tunazidi kuwakaribisha wateja wetu ili wajionee huduma bora zitolewazo na benki yetu na pia tunatoa huduma mbalimbali zikiwemo za Mashine za kutolea fedha(ATM) ambayo hufanya muamala kwa masaa 24,” alisema.

sinzainside
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam, Salie Mlay (kati) akimwelezea Afisa Utumishi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Godfrey Mugomi (pili kushoto) huduma mbali mbali zitolewazo na tawi jipya la NMB Sinza

Ufunguzi wa tawi hili la Sinza unafanya idadi ya matawi yaliyopo Kanda ya Dar es Salaam kufikia ishirini na tatu. Hivyo basi, kuifanya NMB kuendela kuwa benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania.

Tawi hili linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa NMB kama mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu, kufungua akaunti, kuweka na kutoa fedha nk, pia litakua linafunguliwa Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni ( 2:30 asubuhi – 10:30 jioni) na Jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (2:30 asubuhi- 6:30 mchana), Jumapili na siku za Sikukuu hakutakuwa na huduma ndani ya tawi hili.

_DSC4609
Sehemu wa wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo

Akizungumza kwa upande wake wakati wa ufunguzi huo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Afisa Utumishi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Mugomi aliipongeza benki ya NMB kwa kutambua umuhimu wa huduma za kifedha na kusogeza karibu na jamii ili iweze kufaidika na kuwataka wananchi na wateja wapya kutumia tawi hili pekee katika eneo hilo ili kupata huduma za kibenki badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye matawi yaliyo mbali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents