Burudani

Flora Mvungi: Nilianza muziki kabla ya movie, narudi kwenye muziki rasmi

Msanii wa filamu, Flora Mvungi amesema hajaingia kwenye muziki kwa kubahatisha kwanini alianza kuimba hata kabla watu hawajamfahamu kupitia filamu. Tayari ameachia wimbo wake mpya uitwao ‘Kidogo’ aliomshirikisha mume wake H.Baba.

Frola-Mvungi.JPG-2

Flora ameiambia Bongo5 kuwa kabla ya kuingia kwenye filamu, sanaa ambayo aliyokuwa anaipenda ni muziki ambayo kwa wakati huo alishindwa kuingia.

“Muziki nilianza tangu sijaingia kwenye movie,” amesema. “Kipindi ninasoma nilikuwa ninaimba na akina Kala Jeremiah, akina Chidi Benz, ndio wanajua vizuri safari yangu ya muziki ilianzia wapi. Halafu baadaye nilipomaliza shule nikajikuta baadaye ninaingia kwenye maigizo lakini kazi ambayo nilikuwa naipenda ni muziki. Kwahiyo movie ilikuwa kama njia fulani ili nitoke na niweze pata connection na watu mbalimbali na wadau, lakini baadaye nikaja nikatoa single ya kwanza baada ya hapo masuala ya mahusiano yakaanza na masuala ya kulea yakaingilia. Lakini sasa hivi ninamshukuru Mungu mwanangu ameshakuwa sana. Kwahiyo nimerudi tena kwenye muziki rasmi. Sio kwamba nimetoa nyimbo halafu nipotee tena, itakuwa natoa nyomba moja baada ya nyingine pamoja na video,” amesema Mvungi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents