Burudani

Chege: Nitaendelea kufanya video na directors wa Bongo mpaka watu waelewe

Msanii wa muziki kutoka TMK, Chege Chingunda amesema ataendelea kufanya video na waongozaji wa ndani pamoja na watanzania kushindwa kuthamini video za wasanii zinazotengenezwa na waongozaji hao wa nyumbani.

Chege

Chege ameiambia Bongo5 kuwa hata Nigeria ambao wanaonekana wapo juu barani Africa, walianza kujulikana ndani ya nchi yao baada ya wananchi wao kuwasupport ndipo walipopata fursa ya kwenda mbele zaidi.

“Nitaendelea kufanya na director wa bongo mpaka watanielewa,” amesema Chege. “Mimi hainivunji moyo kwasababu naamini siku moja watanzania watakapoamini kazi zetu ndipo zitakuwa na uhai wa kwenda mbali zaidi. Sasa hivi nitajitahidi kubuni vitu vipya kwenye video zangu, kitu cha msingi ni kuwa creative tu,” ameongeza.

“Huwezi kutegemea director akusambazie nyimbo, wewe mwenyewe inabidi utafute connection. Nigeria walianza kutoka kutokana na wenyewe kujitoa hawaendi kufanya video nje ya Nigeria wamefanya video na directors wao na wakaeleweka mbali zaidi. Baada ya kupewa nguvu waongozaji wao wakanunua vifaa vya kuweza kufanya kazi kiubora zaidi. Kwahiyo sisi tunatakiwa tuwasupport madirector wetu, tutakuwa tunawapa nguvu ya kununua vifaa zaidi na tunaweza kwenda sambamba, haishindikani kununua vifaa ambavyo vinafaa kufanya video iwe quality. Kwahiyo tutoe support na wao wataweza kuwekeza zaidi. Lakini tukiwavunja moyo hawawezi kununuA vifaa, hawazezi kuwekeza. Kwahiyo sisi ndo tunatakiwa kuwapa moyo zaidi ili waweze kufanya kazi ambazo zina ubora zaidi.”

Katika hatua nyingine Chege amesema video yao mpya ‘Wauwe’ iliyoongozwa na Adam Juma, imemgharimu jumla ya shilingi milioni 10.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents