Burudani

Amini: Nataka mke wangu ajifungue mtoto wa kiume ili awe mwanasheria

Msanii wa muziki Amini ambaye mke wake ni mjamzito amesema kuwa anaomba mke wake ajifungue mtoto wa kiume ili mwanae aje kuwa mwanasheria na sio mwanamuziki.
Katikati ni msanii wa muziki Amini akiwa na mke wake pamoja na mtu wao wa karibu
Katikati ni msanii wa muziki Amini akiwa na mke wake pamoja na mtu wao wa karibu
Akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe za kuagwa na wanafunzi wenzake wa THT pamoja na uongozi wa taasisi hiyo, Amini alisema anashukuru ndoa yake imejibu na sasa mke wake ni mjamzito. “Mke wangu akijifungua salama nataka mtoto wa kiume ili aje kuwa mwanasheria, sio mwanamuziki,” alisema Amini huku akionyesha kuwa mwenye furaha.

Baada ya kauli hiyo mke wa Amini aitwaye Namcy alizungumza na Bongo5 kuhusu mafanikio aliyoyapata ndani ya ndoa yao.
Mke wa Amini
Mke wa Amini, Namcy

“Inshallah mwenyezi Mungu amenijalia nimeingia kwenye ndoa hata mwaka haujaisha lakini Mungu amenijalia matunda ya ndoa yamepatikana,” alisema. ‘Siwezi kusema mimba ina miezi mingapi lakini inshallah Mungu akitujalia ndani ya mwaka huu unaweza mkasikia kitu. Siku zote watu wanasema ladies first lakini mimi nasema mume wangu awe mtu wa kwanza kuchagua nini anataka hata katika vitu vyangu ninavyotaka kufanya lazima nimshirikishe kwanza mume wangu. Ndoto yake anataka mtoto wake awe mwanasheria,” aliongeza Namcy.

Pia Namcy alisema tangu waingie kwenye ndoa yao rasmi bado hawajakutana na changamoto kubwa ya kuwayumbisha.

“Ndoa yetu ndo tunakaribia kutimiza mwaka mmoja, ninachoweza kusema mume wangu na mimi tulivyokutana nahisi yeye alikuwa ameshamaliza na mimi nimeshamaliza mambo ya ujana. Kwahiyo kulikuwa hakuna kipya ambacho yeye hakijui katika ujana na mimi sina kipya ambacho mimi sikijui katika usichana,” alisisitiza. ‘Mimi naweza kusema Amini ni mtu mwenye mapenzi, kwa sababu mwenyewe ananipenda acha ule upendo tunaosema niwa mke na mume, acha ule upendo wa kibinadamu saa nyingine ananionyesha mimi kama mkewe. Amini ni mtu anayependa kusaidia kila mtu hana ile wanasema ana roho ya korosho ni mtu safi na hana kauli chafu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents