Habari

Arusha mpoo-12-12-12 Ni Wiz Khalifa Day Jijini Pittsburgh, iwe funzo kwa mamlaka nyingine


Labda leo tutaweza kuelewa namna produza mkali wa Bongo P Funk majani alivyo mbele ya wakati, Hii inatokana na kitendo chake cha kuandaa project ambayo aliipa jina la No Name na ku spare a very special date (tarehe 12-12-2012 kama siku rasmi ya kuachia project hiyo.
Mpaka inafika jana si watu wengi waliweza kubashiri namna siku hiyo ilivyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na watu wengi zaidi duniani kubariki ya kwao. Kadi nyingi, na ujumbe mwingi wenye ubunifu wa aina mbali mbali ulitumwa kupitia mitandao ya kijamii iwe Facebook au Twitter.
Sasa kule Marekani katika jiji la pili kwa ukubwa katika mji wa Pennsylvania, Pittsburgh msanii wa Hip Hop Cameron Jibril Thomaz ambaye anajulikana zaidi kama Wiz Khalifa alitunukiwa tuzo ya heshima kwa mchango wake kwa kuli promote jiji hilo kupitia nyimbo zake.
Sherehe hiyo iliandaliwa maalum na Halmashauri ya mji wa Pittsburgh na kuitamka rasmi siku ya tarehe 12 –Dec kuwa ni official Wiz Khalifa Day kama sehemu ya kuonyesha heshima na shukrani kwa msanii huyo kwa mchango wake wa kulitangaza jiji hilo ambalo yeye ni mzaliwa.
Akiongea wakati wa sherehe hizo msanii Wiz Khalifa alishukuru kwa kupata heshima hiyo na kusema ni faraja sana kwake kwani tangu akiwa mdogo aliamini na kutamka kwa wenzake kwamba anatokea Pittsburgh na kwa kupewa heshima hiyo ni jambo la heshima kubwa sana kwake .
Katika sherehe hiyo msanii huyo aliandamana na Mchumba wake Amber Rose, Mama yake na Babu yake ambao nao walipewa heshima ya kutambuliwa rasmi na mamlaka za mji wa Pittsburgh.
Hapa pia nilipata kukumbuka namna mgogoro wa wasanii wa Arusha na mamlaka za mji huo ulivyotokea wakati wa sherehe za kulipa hadhi ya jiji mji wa Arusha. Kwani mamlaka husika ziliwatenga wasanii ambao wametoa mchango mkubwa kulitambulisha jiji hilo katika tenzi na ghani zao na badala yake kumwalika msanii Diamond kutoka Dar-Es-Salaam.
Well wake up guys mamlaka zijifunze kutoka kwa tukio hili. Tuwaenzi wasanii wetu kabla hawajakufa.
Angalia official video ya sherehe ya kupewa heshima Wiz Khalifa katika terehe 12 mwezi wa kumi na mbili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents