Habari

ATCL yatakiwa kubadili mfumo wa uongozi

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ametoa miezi mitatu kwa bodi ya shirika la ndege Tanzania, ATCL kuunda uongozi mpya.

picha-1

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kutambulisha bodi hiyo, amesema uteuzi wa bodi hiyo utasaidiA kuleta tija na ufanisi wa shirika hilo ambalo kwa kipindi kirefu lilikuwa na changamoto nyingi.

“Nataka kuona mabadiliko makubwa katika menejimenti hadi uongozi wa chini, hakikisheni mnaweka uongozi ambao unafuata maadili, utakuwa na ufanisi, ubunifu wa kasi katika utendaji kazi,” alisema.

Aidha Profesa Mbarawa ameitaka bodi hiyo kusimamia na kuboresha mpango wa kibiashara wa usafirishaji katika shirika hilo ili kuweza kumudu soko la ushindani na kuweza kuongeza mapato ya shirika hilo.

“Kama mnavyojua usafiri wa anga una ushindani mkubwa, hivyo ili serikali iweze kupata faida katika biashara hii ni lazima tuboreshe mpango wa kibiashara unaoendana na wakati,” alisisitiza.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents