Burudani

Audio: Kusaga aeleza jinsi Wyclef Jean alivyoomba kushirikiana na Clouds Media

Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema rapper mwenye asili ya Haiti, Wyclef Jean alimtafuta baada ya kusikia kuwa kampuni hiyo imeingia kwenye mfumo mpya wa utangazaji duniani uitwao (Over-the-top content au OTT). Kampuni hiyo imekuwa ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki kufanya hivyo.

WYCLEF22

“Wyclef baada ya kupelekewa habari ya sisi kupeleka OTT ya Afrika alitutafuta,” Kusaga amesema leo kwenye mahojiano aliyofanyiwa kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM.

“Nilitafutwa mimi kwenda kumuona. Kwahiyo mazungumzo hayo tena ni njia nyingine ya kuwasaidia vijana wa Kitanzania. Lakini yeye (Wyclef) anakuja kwa masuala ya publishing. Vijana wengi hawajui kuhusu publishing,” amesema.

“Siwezi kutaja lakini niliwauliza wasanii wawili watatu ‘do you know anything about publishing’ hawajui. Lakini kuna rights nyingine anaweza akawa na publishing rights ambazo zikamsaidia yeye kwenye connection ya sinema, Hollywood wapi wanataka sinema ya Kiswahili, nyimbo ya Kiswahili iingie kwenye Hollywood, ni hela mpaka anakufa,” ameongeza Kusaga.

Katika hatua nyingine, Kusaga amewataka wasanii wa muziki kuongeza bidii, kuwa na nidhamu na kuacha kulalamika kwa kila kitu.

Msikilize hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents