Habari

Baada ya Intercontinental na Club Laaziz sasa Clouds Media yaja na Escape Two

Joseph Kussaga (kushoto) akiwa na Mtangazaji wa Clouds FM, Gerald Hando kwenye Fiesta Dar, 2012.
Mjasiriamali, Mkurugenzi mtendaji na mmiliki wa kampuni ya Clouds Fm Joseph Kusaga anajipanga kuja na kiota cha nguvu cha starehe, chakula na burudani kwa staili ya Lounge ama Mini Club ambacho kinatarajiwa kuwa maeneo ya Safari Carnival karibu kabisa na makao makuu ya Clouds Media.

Kwa mujibu wa Super Snoop wetu baada ya Clouds kujaribu kupiga muziki katika viota mbali mbali kama Intercontinental jijini Dar-es-Salaam na Club Laaziz jijini Dodoma sasa ameamua kuja na Escape Two Mbezi, ambayo tayari inafanya kazi huku Escape Two ambayo ipo pale Safari Carnival iliyopo kwenye hatua za mwisho mwisho za ukamilishaji wa matengenezo ikisemekana kuwa ndio itakayokuwa kiota kikuu cha burudani.

Super Snoop wetu alitonya baada ya kuyasikia matangazo ya Escape Two mara kwa mara kupitia Clouds FM aliamua kutaka kujua inakuwaje kuhusiana na kiota hicho ambacho yeye anasema alifanikiwa kupata habari ya kiota hicho.

Pia habari mahsusi zilizoifikia meza yetu zinadai kuwa Mkurugenzi huyo wa Clouds Media atakuwa redioni siku ya ijumaa ya wiki hii, bado haijajulikana ataongelea nini hasa, lakini inawezekana akatoboa siri hiyo…just watch this space.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents