Michezo

Batista amzimisha mkongwe Ric Flair katikati ya Birthday yake, atuma ujumbe wa vitisho kwa Triple H (+video)

Mchezaji mkongwe wa mchezo wa mieleka nchini Marekani, Ric Flair (70) amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na Batista kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya WWE.

Tukio hilo limetokea jana usiku wa kuamkia leo Februari 26, 2019, ambapo mchezaji huyo mkongwe alikuwa akisherehekea kutimiza miaka 70.

Triple H ndiye aliyekuwa mshehereshaji kwenye tukio hilo, ambapo ulipofika muda wa kumuitwa Ric Flair jukwaani alifanya hivyo, lakini hakutokea kwa muda wa dakika 2.

Ukumbi wote ulikaa kimya ukimsubiria apande jukwaani, na ndio baadae Triple H akaamua aanze aingia back stage kujua amepatwa na msala gani.

Triple H alimkuta Ric Flair ameshachakazwa na walimchukua na kumpatia huduma ya kwanza.

Tukio hilo linajiri katika kipindi ambacho Batista amepangiwa mchezo na Triple H, na inaelezwa kuwa amefanya hivyo kwa lengo la kumtisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents