Bongo Movie

Batuli kumpeleka Ray Kigosi kwenye vyombo vya sheria

Msanii wa filamu, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amesema ni muda mrefu amekuwa akivumilia maneno ya dharau aliyokuwa akijibiwa wakati akihitaji malipo yake kwa msanii mwenzie Vicent ‘Ray’ Kigosi.
Batuli na Ray

Akizungumza kupitia kipindi cha Twenzetu cha Times Fm, Batuli amedai kuwa pesa anayomdai Ray ni milioni 1 na laki 2, malipo halali kwa vipande alivyoshiriki kwenye filamu ya Ray.

“Nikimpigia anaesema ana pesa, namwambia ungekuwa unahela usingeniita kwenye kazi yako.” alisema Batuli

Aliongeza, “Mi nikapata accident ya moto, nikamwambia naomba pesa yangu, akasema njoo upige picha ya ‘Cover’ nikasema sipigi mpaka unipe pesa yangu akanijibu ‘unaumwa wewe’, uvumilivu umefika kikomo nimeamua nitafute msaada wa kisheria na mkataba wangu umeungua kwenye ajali ya moto.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents