BurudaniUncategorized

Belle 9 adai brand yake inamfanya achague show za kufanya

Msanii wa muziki, Abelnengo Damien ‘Belle 9’ amefunguka kwa kudai kuwa kwa level aliyofikia kuna baadhi ya show ambazo hawezi kuzifanya katokana na namna alivyoijenga brand yake.

Belle 9

Muimbaji huyo amedai anatengeneza brand ambayo itakuwa ikielezea aina ya show ambazo anafanya.

“Kitu kikubwa ambacho nakiangalia kwa sasa hivi ni kile ambacho nilikikosa kipindi cha nyuma wakati nipo mwenyewe. So sasa hivi nipo chini ya management na kitu kikubwa ambacho nakiangalia ni profile, kwa sababu kazi nzuri tumeshafanya na watu wamekubali. Kwahiyo kwa sasa ni ile tu package yangu kwamba mtu akimsikia Belle 9, kwenye mawazo yake ni kitu gani anakifikiria ndio kitu ambacho tunajaribu kuki-push sasa hivi,” Belle 9 alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.

Aliongeza, “Kwahiyo unaweza kusikia ngoma nizafanya vizuri, watu wanapiga simu lakini kwa utaratibu ambao tumeuweka na ambavyo tunataka Belle 9 afanye show. Watu wajue Belle 9 anafanya show za aina gani, Belle anafanya show za class gani, unajua kuna class ya juu, ya chini na katikati. Kwahiyo kama msanii ni uwamuzi wako kuamua nijiweke kwenye class ipi. kwa hiyo ndio hicho ambacho kwa sasa hivi tunakiangalia. Hatuangalii ngoma nimetoka tu tunarudisha vipi faida katika pesa ambayo tumetumia ila tunaangalia kitu gani kinaweza kututoa hapa tulipoishia kwenda sehemu nyingine,” 

Video ya muimbaji huyo ya wimbo ‘Give It To Me’ aliyomshirikisha G-Nako, imeangaliwa mara 1,046,369 kupitia mtandao wa YouTube kwa kipindi cha miezi 4.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents