Burudani

Ben Pol aeleza kwanini alishindwa kumaliza chuo

Mwimbaji wa R&B, Ben Pol ameweka wazi sababu iliyomfanya kushindwa kuendelea na masomo yake ya biashara kwenye chuo cha IFM.

12080513_170899806587110_7547465_n

Akizungumza na Global TV hivi karibuni, Ben Pol alisema muziki umemfanya ashindwe kufuatilia masomo yake vizuri.

“Nilikuwa nasoma IMF, Banking Finance Diploma,” alisema. “Nilisoma mwaka mmoja na baada ya hapo mambo yakawa mengi, tour nikasafiri kwenda Ujerumani nikarudi hapa nikakutana na tour kama mikoa kumi, nikashindwa ku-manage vizuri chuo, nikasitisha.”

“Mwaka huu pia nikaanza Open University, Open University nilitaka kuchukua International Business, ile kuchukua tu application nimechukua na notes nikapata safari nyingine Coke Studio, nikapata na tour nyingine tena, kazi zikawa nyingi sana, nikasitisha tena mwaka huu.

“Nina mpango wa kuendelea, natafuta nanma ya kuendelea na kufanya vitu viwili kwa pamoja,” alieleza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents