Burudani

Ben Pol apoteza ‘flash disk’ yenye kazi zake za muziki

Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol amepoteza ‘flash disk’ ambayo ndani yake kulikuwa na nyimbo ambazo mipango yake ilikuwa bado.
Ben-Pol

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video ya wimbo ‘Ningefanyaje’ akiwa amemshirikisha Avril kutoka Kenya, ameiambia Bongo5 kuwa tayari ameanza kupata madhara kutokana na kupotea kwa flash hiyo.

“Flash niliyopoteza tayari imeanza kuniaribia ratiba yangu, kuna nyimbo ambayo nilifanya na Jux nimeanza kutumiwa kwenye magroup ya whatsap na hatukuwa na mpango nayo kwa sasa. Pia kulikuwa na nyimbo zangu ambazo zilitakiwa ziingie kwenye albamu yangu mpya nazo natumiwa. Kwahiyo kwa ufupi tu, mambo hayako sawa kwa sababu nyimbo zangu zinazagaa bila mpango,” alisema Ben Pol.

Ben Pol alipoteza flash yake hivi karibuni akiwa katika eneo ya Mlimani City.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents