Burudani

Ben Pol kupeleka muziki wake Europe, USA na China (+video)

Msanii wa muziki Bongo, Ben Pol ametangaza tour yake ambayo itapita katika nchi mbali mbali.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Zai’ amesema tour hiyo inakuja baada ya kufanya tour kadhaa Bongo kama Sophia Tour na Moyo Mashine Night.

“Pia mwaka huu nitafanya tour lakini nataka kutoka kidogo, ni nje ya Tanzania nitaenda Europe, USA, nitakuwepo pia Kenya, halafu China,” Ben Pol ameiambia Bongo5.

Utakumbuka hivi karibuni Vanessa Mdee na Jux walitangaza tour yao’ In Love & Money’ ambayo itapita katika mikoa kama Mwanza, Arusha, Mtwara, Dar es Salaam n.k.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents